Waziri wa habari utamaduni na michezo ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa CCM Bara George Mkuchika amewataka wanachama wenzake wa chama cha Mapinduzi CCM kutumia vikao vya chama kumaliza tofauti zao badala ya kulumbana kupitia vyombo vya habari.

Alikuwa akizungumza katika kipindi cha MIMI NA TANZANIA kilichorushwa machi 28 mwaka huu katika Luninga ya Chanel 10 kuanzia saa 10:30 – 11:00 Jioni wakati mwandishi na mtangazaji wa kipindi hicho Cyprian Musiba kwa kushirikiana na kada wa CCM Violet Elias walipotaka kujua maoni na mtazamo wake kuhusiana na hali ya siasa hapa nchini.

Mkuchika amekemea vikali tabia ya wana-CCM wenye dhamana serikalini na wasio na dhamana serikalini kulumbana huku wakijua fika kwamba kuna mahali ambapo wanaweza kuzungumza kwa kirefu zaidi bila kuleta hofu kwa wananchi na wanachama wa CCM.

Amesema hata mwasisi wa taifa hili baba wa taifa hayati mwalimu Nyerere alikuwa mara zote katika hotuba zake akisisitiza wanachama wa CCM wanaotofautiana kwa mawazo kumaliza tofauti hizo kupitia vikao vya chama.

Aidha amebainisha hiyo  njia pekee ambayo inaweza kuleta umoja na mshikamano ndani ya chama ni vikao kuliko sasa ambapo kila mwanachama wa CCM ili mradi anajua kuna vyombo vya habari anakwenda kutumia vyombo hivyo kumtukana yule ambaye anahisi ni mbaya wake ndani ya CCM.

Hivi karibu kumekuwa na malumbano yasiyo na msingi kati ya Mbunge wa Kyela CCM Harison Mwakyembe na Mbunge wa Igunga CCM Rostam Azizi wakituhumiana kuchafuana katika vyombo vya habari,malumbano ambayo yanaonekana kuwa yanaathari ndani ya chama na nje ya chama kwa wanachama wa cha hicho tawala na wananchi kwa ujumla.

Advertisements
Posted by: chtentv | March 6, 2009

Maskini Wema Sepetu!!

[Wema++1.JPG]

Mrembo wema sepetu akipewa pole na rafiki yake baada ya kuachiwa kwa dhamana leo mahakamani kinondoni anakikabiliwa na shtaka la kuharibu gari la mwigizaji steve kanumba. mrembo huyu aliyepata kuwa miss tz alikuwa rumande toka wiki iliyopita baada ya kukosa dhamana alipofikishwa kizimbani kwa mara ya kwanza
mama mzazi wa wema sepetu akisaidiwa na nduguye wa kiume ilibidi watumie nguvu wema aondoke nao wao na sio rafikiye ambaye alifika hapo mahakamani

Posted by: chtentv | February 4, 2009

Nauli za Treni zapanda

Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) imetangaza kupandisha nauli za treni za abiria kwa asilimia 11.6 kwa madaraja yote kuanzia Februari 15 mwaka huu. Nauli hizo zilizoidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) zitatozwa kulingana na umbali wa kituo hadi kituo kati ya Dar es Salaam na Kigoma na ya chini itakuwa Sh 6,200 na ya juu itakuwa Sh 60,600.

Taarifa ya uongozi wa TRL kwa umma imeeleza kuwa kiwango hicho kipya cha nauli hakitahusisha huduma mpya ya daraja la tatu zinazotarajiwa kuanza Februari saba mwaka huu. Kwa mujibu wa tangazo la kampuni hiyo iliyo chini ya uongozi wa Kampuni ya Rites ya India, abiria wa daraja la tatu watalipa kati ya Sh 6,200 na Sh 19,200, daraja la tatu kulala watalipa kati ya Sh 7,700 na Sh 24,000.

Daraja la pili kulala watalipa kati ya Sh 13,300 na Sh 44,400 na daraja la kwanza kulala watalipa kati ya Sh 16,900 na Sh 60,600. Awali abiria waliosafiri kwa mabehewa ya daraja la tatu walilipa kati ya Sh 3,300 na 17,100, daraja la pili kati ya Sh 3,400 na Sh 39,700 na daraja la kwanza walilipa kati ya Sh 7,600 na Sh 54,300 kwa kuzingatia umbali wa kituo anachoanzia safari hadi anapoteremkia.

Nauli mpya zilizotajwa katika taarifa hiyo, zinahusu Kituo Kikuu cha Dar es Salaam kwenda Morogoro, Dodoma, Tabora, Isaka, Shinyanga, Mwanza, Urambo, Kaliua, Nguruka, Uvinza na Kigoma. “Nauli mpya ya daraja la tatu kulala ni za kuanza tu. Haya mabehewa yaliyoingizwa nchini hivi karibuni yatatumika kwa huduma za abiria za treni za moja kwa moja ‘Express’ tu hakuna ongezeko la nauli katika huduma hiyo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa TRL, treni hizo za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma na Mwanza zitakuwa za aina mbili kwa kutumia mabehewa ya daraja la tatu kulala. Kampuni hiyo ilisema, treni hizo zitapunguza muda wa safari kwenda na kurudi kwa saa nne na zitaondoka Dar es Salaam kila Jumanne na Ijumaa kwenda Kigoma na Mwanza na kila Jumapili kwenda Kigoma.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa, treni za Express zitakuwa zikiondoka Dar es Salaam kila Jumatano kwenda Kigoma tu, na kila Jumamosi itatoka Dar es Salaam kwenda Mwanza tu, saa 11 jioni. TRL ilieleza kuwa treni za abiria za moja kwa moja zitasimama katika vituo vya Morogoro, Kilosa, Dodoma, Saranda, Manyoni, Tabora, Urambo, Kaliua, Nguruka, Uvinza, Kigoma, Isaka, Shinyanga na Mwanza.

“Abiria ataruhusiwa kuchukua mzigo wake binafsi usiozidi kilo 30 katika huduma za treni za abiria za moja kwa moja ‘Express Train Service’, ambazo mabehewa ya daraja la tatu kulala yatatumika,” ilisema taarifa hiyo na kubainisha kwamba, kuanzia Machi mosi mwaka huu, huduma ya treni ya abiria ya Jumapili kwenda Kigoma itatumia mabehewa ya daraja la tatu kukaa. TRL ilianza kutoa huduma za reli Oktoba mosi mwaka juzi baada ya kusaini makubaliano na serikali Septemba tatu mwaka huo, kuiruhusu Kampuni ya Rites kutoka India kuchukua majukumu ya Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Posted by: chtentv | January 30, 2009

When the Pm cries..

Prime Minister Mizengo Pinda was yesterday moved to tears on the floor of Parliament in Dodoma, on being asked to explain his recent remark that those responsible for the ongoing brutal ritual killings of albinos in some parts of the country must also be killed.

“It is really painful to witness the brutality being committed against the albinos. This is pure murder. As a nation, we can no longer tolerate this,” he said, before taking off his spectacles to wipe his tears.

Mr Pinda broke down when responding to a question by the Leader of the Opposition in the House, Mr Hamad Rashid Mohammed.

The Civic United Front MP for Wawi had sought a clarification from the Premier on reports that he had said during a recent public rally that people caught red-handed killing albinos should also be killed on the spot.

Speaking during the PM’s Question Time, a visibly emotional Mr Pinda defended his statement, saying: “I seek forgiveness from God if what I said is worse than what the killers of albinos are doing to their fellow human beings.”

Mr Mohammed, describing the statement as an extrajudicial order, said it could undermine the rule of law and good governance.

In his clarification, Mr Pinda did not deny issuing such a statement, but said that it had be misinterpreted.

He said his only intention was to show the seriousness with which the Government was addressing the albino killing menace.

Categories