Mimi na Tanzania

Wiki Hii Katika Mimi Na Tanzania

Cyprian Musiba

Cyprian Musiba

Ni kipindi kinachozungumzia juu ya hali halisi ya maisha ya Mtanzania katika ngazi ya kiuchumi,kisiasa na kimazingira na kiutamaduni. Kipindi hiki kinaendeshwa na Mtangazaji Cyprian Musiba,kila siku ya jumamosi muda kuanzia saa 10:30 jioni HAPA CHANEL 10.

Katika kipindi hiki utaona wageni mbalimbali wa rika mbalimbali, kama vile wanasiasa,wataalam wa uchumi,wananchi wa kawaida,vijana, akina mama kwa ujumla wao,walemavu wa aina mbalimbali,wanafunzi nk.

ssm111831

Wiki hii katika kipindi cha MIMI NA TANZANIA tutazungumza ana kwa ana na waziri wa habari na utamaduni na michezo George Mkuchika. Katika kipindi hicho kitakachorushwa hewani Jumamosi Machi 28 saa kumi na nusu jioni pamoja na Aprili 4. MH.waziri atazungumzia juu ya vyombo vya habari na changamoto zake pamoja na mswada unaohusu vyombo vya habari utakaowasilishwa Bungeni tayari kwa kujadiliwa mapema mwaka huu. Aidha pia mheshimiwa atazungumzia juu ya malumbano ya wanasiasa hususani wale wabunge wa chama tawala CCM ambao wamekuwa wanalumbana kupitia vyombo vya habari.

Mkuchika Awaasa Wana-CCM Wenzie Kutumia Vikao vya Chama Kumaliza Tofauti Zao

Waziri wa habari utamaduni na michezo ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa CCM Bara George Mkuchika amewataka wanachama wenzake wa chama cha Mapinduzi CCM kutumia vikao vya chama kumaliza tofauti zao badala ya kulumbana kupitia vyombo vya habari.

Alikuwa akizungumza katika kipindi cha MIMI NA TANZANIA kilichorushwa machi 28 mwaka huu katika Luninga ya Chanel 10 kuanzia saa 10:30 – 11:00 Jioni wakati mwandishi na mtangazaji wa kipindi hicho Cyprian Musiba kwa kushirikiana na kada wa CCM Violet Elias walipotaka kujua maoni na mtazamo wake kuhusiana na hali ya siasa hapa nchini.

Mkuchika amekemea vikali tabia ya wana-CCM wenye dhamana serikalini na wasio na dhamana serikalini kulumbana huku wakijua fika kwamba kuna mahali ambapo wanaweza kuzungumza kwa kirefu zaidi bila kuleta hofu kwa wananchi na wanachama wa CCM.

Amesema hata mwasisi wa taifa hili baba wa taifa hayati mwalimu Nyerere alikuwa mara zote katika hotuba zake akisisitiza wanachama wa CCM wanaotofautiana kwa mawazo kumaliza tofauti hizo kupitia vikao vya chama.

Aidha amebainisha hiyo  njia pekee ambayo inaweza kuleta umoja na mshikamano ndani ya chama ni vikao kuliko sasa ambapo kila mwanachama wa CCM ili mradi anajua kuna vyombo vya habari anakwenda kutumia vyombo hivyo kumtukana yule ambaye anahisi ni mbaya wake ndani ya CCM.

Hivi karibu kumekuwa na malumbano yasiyo na msingi kati ya Mbunge wa Kyela CCM Harison Mwakyembe na Mbunge wa Igunga CCM Rostam Azizi wakituhumiana kuchafuana katika vyombo vya habari,malumbano ambayo yanaonekana kuwa yanaathari ndani ya chama na nje ya chama kwa wanachama wa cha hicho tawala na wananchi kwa ujumla.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: